IRENE PAUL AFUNGUKA:SIBAGUI DINI, KABILA KWENYE MAPENZI
MTOTO mzuri kwenye kilinge cha Bongo Movies, Irene Paul amefunguka
kuwa kwenye suala la uhusiano, hana kipingamizi sana kwani anachoangalia
ni mtu anayempenda haijalishi dini wala kabila.
“Naangalia
tu, mtu anayenipenda ananipenda kweli au anaigiza? Nikigundua
ananipenda kweli, nampenda pia. Hata aweje huyo ndiye atakayekuwa wangu
wa maisha,” alisema Irene.
Irene Paul.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni jijini Dar, Irene alisema
licha ya kuwa bado hajamuanika mpenzi wake lakini suala la dini, kabila
kwake siyo ishu ya msingi zaidi anaangalia mapenzi ya dhati.
Post a Comment