ad

ad

URAIS 2015: Vigogo wa CCM wahojiwa na kamati ya maadili

 
 Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye akiwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma tayari kwa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili.
 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa akizungumza na Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye kabla ya kuanza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma.
Ndugu William Ngeleja akisubiri kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama.
Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa kizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo alisema mazungumzo yalikuwa mazuri,yalikuwa yenye nia ya kukijenga chama kwa ajili ya uchaguzi 2015.
Waandishi wa Habari wakiwajibika kuandika habari nje ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo viongozi watatu walihojiwa na Kamati ndogo ya Maadili.

Kamati ndogo ya maadili ya Chama cha mapinduzi CCM imekutana Mjini Dodoma na kuwahoji wanachama watatu wa chama hicho wanaodaiwa kutangaza nia ya kugombea Urais nakuanza Kampeni za Uchaguzi ujao wa mwaka 2015 kinyume na utaratibu na maadili ya chama hicho.
Kamati hiyo inayoongoza na Mwenyekiti Philip Mangula Makamu wake Abdurahman kinana ,wajumbe William Lukuvi,Maua Daftari,Pindi Chana mtu wa kwanza kumhoji alikuwa ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa aliehojiwa kwa saa moja na Nusu ,na baadaye aliongea na waandishi wa habari.

Na wengine waliohojiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema Wiliam Ngereja ambao hawakuwa tayari kuzungumza na waandishi na kusema kamati hiyo ndiyo yenye jibu sahihi

Baada ya zoezi hilo kukamamilka waandishi wa habari walitaka kupata ufafanuzi zaidi wa mahojiano hayo kwa katibu mkuu wa chama hicho Abdurahaman kinana,yeye hakuwa tayari kuzungumza licha ya kusema kuwa kamati hiyo itaendelea kuwahoji viongozi wengine hapo kesho.

Miongoni mwa wale watakaohojiwa kesho ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na uratibu Steven Wassira,Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe,pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba.

MWISHO.
Powered by Blogger.