WOLPER, ZAMARADI BIFU ZITO
Jacqueline Wolper.
STAA wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper amemrushia maneno ya
lawama Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema kuwa ni
mnafki na adui yake mkubwa katika maisha.
Zamaradi Mketema.
Akizungumza na Amani juzikati, Wolper alisema amegundua kuwa
mtangazaji huyo amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana maisha yake kwa
mtindo wa chanya (negative), akamuomba amuache.“Nilibadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu, Zamaradi akanifuatilia, juzijuzi nimerudi kundini (kwenye Ukristo) kwa kusikiliza maneno ya wazazi wangu, akanifuatilia tena.
Baada ya Wolper kulalamika sana, Amani lilimtafuta Zamaradi kwa njia ya simu ya kiganjani ambapo alisema yeye anawajibika kwa kazi yake hakuna ishu ya kumfuatilia mtu.
“Mimi simfuatilii maisha yake, ni kazi tu. Kama mwandishi wa habari nikipata habari ya mtu natakiwa kubalansi (uwiano) naye,” alisema Zamaradi.

Post a Comment