SHAMSA FORD AGOMA KUOLEWA
STAA wa filamu Bongo ‘Shamsa Ford’ amegoma kuolewa siku chache baada
ya tarehe ya harusi yake kufika kwa madai kuwa mambo yalivyopangwa sivyo
alivyotarajia.
Shamsa Ford.
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika, zinasema kuwa harusi ya
Shamsa ilikuwa ifanyike kati ya Desemba 24 na 25, mwaka huu lakini
aligoma kwa vile walikwenda kinyume na makubaliano ya tarehe husika.
“Unajua mwanzoni tarehe ilipangwa nyingine na Shamsa alijiandaa kwa
siku hiyo, lakini wanafamilia ya mumewe mtarajiwa wakataka tarehe
ibadilishwe ili wafunge siku moja na kaka wa mumewe mtarajiwa yaani
shemeji yake ambaye naye pia alikuwa anaoa.
“Ndoa ya shemeji yake ilitakiwa kuharakishwa kwa sababu mchumba wake
ana mimba tayari. Kwa hiyo sasa wanafamilia wakaona ni bora kufanya
shughuli ya pamoja kwa kuwa wote ni ndugu.. Shamsa akagoma, akataka
tarehe ileile waliyokubaliana,” kilieleza chanzo chetu.
Shamsa alipatikana kwenye simu na kufafanua ambapo alisema: “Mimi sikutaka mambo ya kuchanganya harusi mbili kwa wakati mmoja.
Ukizingatia hii ni ndoa yangu ya kwanza halafu leo hii eti
tukafanyiwe shughuli pamoja, nitakosa uhuru na sherehe yangu. Mimi nina
marafiki wengi ambao wameipania siku hiyo, ndiyo maana niliomba wao
waoane kwanza siku hiyo sisi tupange tu mwakani.”

Post a Comment