OKWI ATUA YANGA SC
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KLABU
ya Yanga SC ya Dar es Salaam imemsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba
SC, Emmanuel Arnold Okwi raia wa Uganda kwa Mkataba wa mia miwili na
nusu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb
amesema jioni hii mjini Dar es Salaam kwamba wamemsajili Okwi na ataanza
kuichezea timu hiyo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na michuano ya
Afrika.
Etoile
du Sahel ya Tunisia ilimnunua Okwi kutoka Simba SC Januari mwaka huu
kwa dola za Kimarekani 300,000, lakini mchezaji huyo akaamua kuachana na
klabu hiyo na kurejea kupumzika kwao Uganda, kwa madai hakulipwa
mishahara kwa miezi mitatu.
Wakati
huo huo, Etoile hadi sasa haijailipa Simba SC fedha zake za kumnunua
mchezaji huyo na sakata lake limefikishwa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA).
Baada
ya Okwi kukaa bila kucheza kwa miezi sita, Shirikisho la Soka la Uganda
(FUFA) lilimpigania aruhusiwe kurejea nyumbani kuichezea SC Villa ya
huko ili kunusuru kiwango chake.
Hata
hivyo, baada ya kung’ara na timu ya taifa ya Uganda ‘The Ceanes’ nchini
Kenya kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Challenge mwezi huu , Okwi anasajiliwa Yanga SC.
Bin
Kleb amesema kwamba walimsajili Okwi tarkiban siku sita zilizopita,
lakini Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) imepatikana leo na ndiyo
maana wameamua kumtangaza.
“Amesaini
mkataba kiasi cha siku sita zilizopita, ila taratibu za uhamisho
zimekamilika leo. Atakuwa nasi kwa misimu miwili na nusu ijayo,”alisema
Bin Kleb.
Alipoulizwa
kuhusu utata wa sakata lake ambalo limefika hadi FIFA, Kleb alisema;
“Tumefuatilia kote, hadi kwa wanasheria, na tumefanikiwa kupata hadi ITC
yake, nawaambia mashabiki wa Yanga wajue viongozi wao wanafanya kazi,
hatuna stori nyingi, sisi tunafanya vitendo, tunafanya kazi kwa siri
sana,”.
“Na
tumepitia sehemu zote, tumeona kabisa tuko sahihi katika kumsajili
mchezaji huyu na hakutakuwa na tatizo lolote upande wetu,”alisema.
Bin
Kleb alisema lengo la Yanga SC ni kufanya vizuri katika Ligi ya Mbingwa
Afrika mwakani na ndiyo maana wameamua kuimarisha timu kwa kusajili
wachezaji wazuri.

Post a Comment