MASTAA KUFURIKA... DAR LIVE SIKU YA KRISMASI
Wema Sepetu.
BURUDANI juu ya burudani! Mastaa mbalimbali wa
filamu wanatarajiwa kufurika kwa wingi ndani ya Ukumbi wa Dar Live
Mbagala-Zakhem jijini Dar, siku ya Krismasi katika tamasha maalumu
lililopewa jina la Mtoko wa Mastaa, likiambatana na shoo ya nguvu yenye
mchanganyiko wa Bongo Fleva, Hip Hop na Taarabu kutoka kwa wasanii nguli
wa miondoko hiyo.
Siku hiyo, mashabiki watapata nafasi ya kupiga picha mbalimbali na
mastaa hao sehemu tofautitofauti ikiwemo kwenye zuria jekundu (red
carpet) pamoja na kubadilishana nao mawazo.
Akizungumzia shoo hiyo, Mratibu wa Burudani wa Ukumbi wa Dar Live,
Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, alisema kwa upande wa muziki, wasanii
watakaopanda stejini kuangusha shoo kali na ya kipekee ni pamoja na
Profesa Jay, Joh Makini, huku Kassim Mganga ‘Tajiri wa Mahaba’,
akitarajiwa kuangusha shoo kali kwa upande wa Bongo Fleva.
Aidha, Abby Cool alisema kwa upande wa Taarabu, mfalme wa nyimbo hizo
za mwambao, Mzee Yusuf, atalipamba jukwaa kwa staili ya aina yake
pamoja na Bendi ya Jahazi Modern Taarabu.
“Siku hiyo kutakuwa na mastaa mbalimbali wa filamu, ambapo mashabiki
watapata fursa ya kupiga nao picha sehemu mbalimbali ikiwemo red carpet.
“Hakika itakuwa ni shoo ya aina yake. Kutakuwa na mchanganyiko wa
Bongo Fleva, Hip Hop na Taarabu ili kuwaburudisha wadau na wapenzi wa
burudani,” alisema Abby Cool.
Mbali na burudani hiyo, Abby Cool alisema kutakuwa na michezo
mbalimbali kwa watoto kama kuogelea, bembea za kisasa kabisa pamoja na
mazingaombwe kutoka kwa mtaalamu Profesa Karabash.

Post a Comment