AZAMTV YAPATA LESENI YA KUWA HEWANI RASMI
TCRA yaipa Azam Media leseni kuiwezesha kuendesha shughuli zake.
Azam Media Ltd leo imepata leseni kutoka Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) na hivyo kuwa na uwezo wa kuanza rasmi shughuli zake hapa Tanzania.
Azam Media Ltd leo imepata leseni kutoka Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) na hivyo kuwa na uwezo wa kuanza rasmi shughuli zake hapa Tanzania.
Hatua hii muhimu sasa inaiwezesha AzamTV kuanza kutoa huduma zake kwa
wateja wake kote Tanzania kuanzia tarehe16 Desemba. Huduma hii itwapa
fursa wateja kuangalia zaidi ya chaneli 50 za kitaifa na kimataifa
ziliozosheheni burudani kwa ajili ya familia kwa bei nafuu ya shilingi
12,500/= kwa mwezi. Kutakuwepo wigo mpana wa kuchagua kifaacho kuangalia
vikiwemo vipindi vya michezo, makala, watoto na tamthilia kutoka
Tanzania, barani Afrika na sehemu mbalimbali za dunia. Baadhi ya
vipindi hivyo tajwa vitapatikana katika chaneli maarufu kama vile
National Geographic Gold na Nickelodeon, na pia matangazo yetu yatakuwa
na chaneli za bila malipo zikiwemo TBC1, Channel 10, Clouds, ZBC na K24.
Jambo la kusisimu zaidi ni kwamba AzamTV itakuwa na matangazo katika chaneli zake tatu:
AzamOne
- Itakuwa na vipindi vya kiafrika, ambapo kwa asilimia kubwa vitahusu
masuala ya Afrika Mashariki kwa lugha ya Kiswahili. Hii ndiyo chaneli
ambayo itakuwa ikirusha matangazo ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara;
AzamTwo
– Hapa vitapatikana vipindi vya burudani kwa familia amabavyo ni vya
kimataifa na baadahi ya hiovyo vitakuwa katika lugha ya kiswahili;
SinemaZetu – Chaneli maalum kwa ajili ya tamthilia za kitanzania.
Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema: “Huu ni wakati wa kujivunia kwa Tanzania kwani sasa ina huduma za luninga zinazopatikana kwa bei ambayo wengi wanaweza kuimudu. Miezi michache ijayo tutaivusha huduma hii mipaka hadi katika nchi zingine za Afrika Mashariki na hata mbali zaidi. Nimefarijika kwamba tumewekeza vilivyo katika chombo hiki cha kitanzania na tutaendelea kufanya hivyo”.

Torrington pia alibainisha kuwa kwa wateja ambao hawatapenda kungojea
kuzinduliwa rasimi wa huduma za Azam TV, milango ya ofisi zake za Dar
es Salaam itakuwa wazi kuanzia leo (Ijumaa Desemba 6, 2013). Wateja
wataweza kununua vifaa muhimu kutoka duka la AzamTV na kwa mawakala
walioidhinishwa na hivyuo kuweza kujionea vipindi mbalimbali kuanznia
sasa – japo malipo yao kwa mwezi yatahesabiwa kuanzia Desember 16.

Post a Comment