ARSENAL YAKUTANA NA KIPIGO KILALI
Vinara wa
Ligi Kuu ya England, Arsenal wamekutana na kipigo kikali kutoka kwa Manchester
City cha mabao 6-3 katika mechi iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Etihad jijini
Manchester.
Kutokana na
kipigo hicho Man City imefikisha pointi 32 wakati Arsenal imebaki kileleni
ikiwa na pointi 35.
Mabao ya Man
City yamefungwa na Sergio Agüero katika dakika ya 14, Álvaro Negredo (39),
Fernandinho (50 na 88) na David Silva (66).
Theo Walcott
aliifungia Arsenal mabao mawili katika dakika ya 31 na 63 kisha Per Mertesacker
akaongeza la tatu katika dakika ya 90.


Post a Comment