AMANDA: MWAKA 2013 ULIKUWA MAJANGA KWANGU
MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’
amefunguka kuwa mwaka 2013 ulikuwa majanga kwake kwani ulikuwa mgumu
sana na mambo yake hayakumwendea vizuri.
Akichonga Amanda alisema bora mwaka huu upite, kwani
ulikuwa mgumu sana kwa upande wake katika mambo f’lani ambayo hakutaka
kuyataja ila anaamini kuwa mwaka ujao utakuwa mzuri kwake kwani
ameshaanza kuona dalili za mafanikio mapema.
“Mwaka 2013 ulikuwa mgumu kwangu, ila nashukuru unaisha, ninaamini
huo ujao utakuwa mzuri na wa mafanikio kwangu kwani nimeshaanza kuona
dalili nzuri, suala la kuolewa halipo kichwani kwani hata sina mwanaume
kwa sasa, ninawaza tu jinsi ya kupata fedha kwa kufanya kazi kwa bidii,”
alisema Amanda.
AMANDA POSHY KATIKA POZI

Post a Comment