WASHINDI WA DROO NDOGO YA CHAMPIONI 'SHINDA MAHELA' WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO LEO
Clement Michael (kulia) ambaye ni mkazi wa Mbagala-Zakhem, Dar, akikabidhiwa Sofa Set yake na Mr Championi.
Clement
akichekelea baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya Sofa Set leo nje ya
ofisi za Global Publishers zilizopo Mwenge, Bamaga jijini Dar.
Bashir Hassan (kushoto) mshindi wa friji akikabidhiwa zawadi yake na Mr Championi nje ya ofisi za Global Publishers.
WASHINDI wa Droo Ndogo ya Promosheni ya Shinda Mahela na Championi,
leo wamekabidhiwa zawadi zao nje ya ofisi za kampuni ya Global
Publishers & General Enterprises Ltd wachapishaji wa magazeti ya
Championi, Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda zilizopo
Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa washindi waliofika
kuchukua zawadi zao ni Clement Michael mshindi wa Sofa Set, Bashir
Hassan aliyejishindia Friji na Radephili Mcharo aliyejinyakulia Jezi.
(PICHA NA ISSA MNALLY / GPL)

Post a Comment