Sherehe za miaka mitano ya Usiku wa Khanga za Kale, Nyumbani Lounge Novemba 17
WADAU mbalimbali wanatarajia
kujumuika leo Jumapili jioni Novemba 17, kwenye ukumbi na Mgahawa wa kisasa wa Nyumbani Lounge
kusherekea Miaka Mitano ya Usiku wa Khanga za Kale ‘5th Extra Vaa Khanga Party’
sambamba na shoo kali kutoka kwa Dj Tass.
Akizungumzia mmoja wa waandaji wa
shoo hiyo ambaye pia ni mbunifu na mwanamitindo, Wancy Nells Emmah,
alisema tayari maandalizi yamekamilika na tayari tiketi zinatolewa bure
kwa waalikwa.
“Shoo hii ni ya bure kwa wadau
wa Kanga za Kale, na wengine wote wanaombwa kujitokeza kwa wingi
kuchukua ‘complimentary’ kwenye duka la Fabak Fashion, pale Msasani kwa Mwalimu
Nyerere, au kupitia namba0655999331/au 0713263363 alisema Wancy.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fabak
Fashion na mwandaaji wa onyesho hilo, kila mwaka,
Asia Idarous
Khamsin, alisema wadau hao watajumuika kwa pamoja na kula keki
maalum sambamba na kushuhudia shoo ndogo ya vazi hilo.
“‘ Usiku wa ‘5th Extra Vaa Khanga
Party’, si wa kukosa kwani tutakula keki kwa pamoja, kutoa vyeti maalum vya
shukrani kwa wadau, kucheza mziki na kufamiana kwa pamoja” alisema Asia
Idorous.
Aidha, katika shoo hiyo, Dj Tass wa
24 Djs atatoa burudani kwa wadau watakaojumuika hapo sambamba na surprise
mbalimbali kwa wadau hao ambao watapata kucheza 'Karioki'..

Post a Comment