ad

ad

RAGE AMGOMEA MALINZI, ASEMA HAKUNA MKUTANO SIMBA


MWENYEKITI wa Simba Ismail Aden Rage amesikia taarifa aliyotumiwa na Shirikisho la Tanzania (TFF) la kumtaka kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa klabu hiyo.

Rage ametangaza msimamo wake huo siku ya jana ambapo amesema kamwe hawezi kuafiki kuchukua uamuzi huo kutokana na TFF kuingilia majukumu yake.

Rage amesema katiba ya Simba ibara ya 22 inaeleza wazi kwamba mwenyekiti akishirikiana na kamati yake ya utendaji wanaweza kuitisha mkutano mkuu wa dharura kama wataona kuna haja ya kufanya hivyo.
Amesema hakufurahishwa na uamuzi huo wa TFF ambapo alitegemea kwanza shirikisho hilo kupitia kamati yake ya utendaji inayoongozwa na Rais Jamal Malinzi lingekemea mapinduzi aliyofanyiwa.

“Katiba inatamka wazi mwenye mamlaka ya kuitisha mkutano mkuu ninayo mimi nikishirikiana na kamati ya utendaji na kwa jinsi hali ilivyo sioni haja ya kufanya hivyo, nasema hakuna mkutano,” alisema Rage.
Aidha Rage amesema endapo TFF itaendelea kumlazimisha kufanya hivyo hatasita kuchukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu nafasi yake hiyo.
Powered by Blogger.