MWIGULU NCHEMBA:KUVULIWA VYEO ZITTO KABWE"NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATWALA AKILI KUBWA"
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu.
Kwenye
chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Pale
bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu
waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu.
Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa.
Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa.
Vijana wahitimu wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia
kuhutubia mkutano wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo
inapotawala akili kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa,
Baregu, Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa
chadema ni rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum
wa viongozi ndio utakwepo kwenye list.
I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and consistent
politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi kosa
walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga
watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko
mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko
mafunzoni.
Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi
Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi
CHANZO NI BLOG YA MWIGULU NCHEMBA
Post a Comment