MASOGANGE APIGA ZA UTUPU..BAADA YA KUTOKA LUPANGO.
Agnes Gerald ‘Masogange’ katika pozi.
SIKU chache baada ya kutoka lupango kwa msala wa madawa ya kulevya,
‘video queen grade one’ Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametupia picha
za utupu mtandaoni.
Video queen grade one Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
Masogange
na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5,
mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na baadaye
mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga
waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama
Methamphetamine.

Baada
ya kuachiwa huru, Masogange anayesifika kwa kuwa na figa matata,
alitupia picha hizo katika mtandao wa Instagram akiwa amevalia sidiria
na nguo ya ndani pekee hali iliyowafanya wafuasi wa mtandao huo
wamshangae huku wengi wakimlaumu kuwa alichokifanya hakifanani na
maadili ya Mtanzania.
“Sasa
huu upuuzi gani unatuwekea humu, kwani kila kitu unachofanya ni lazima
sisi tuone? Hivi kwa nini mastaa wa Bongo wanapenda kujirahisi kiasi
hiki?” alihoji mmoja wa wafuasi wa mtandao huo.
Pamoja na wadau
wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange hakujali, aliwajibu kuwa
kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe kwenye listi ya marafiki
mtandaoni humo kwani siyo lazima.
“Hii ni akaunti yangu, nina
uhuru wa kuweka picha za aina yoyote. Kama mtu anaona nimemkera basi
‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya kuogelea sasa mlitaka nivae pensi
niogelee nayo? Simuogopi mtu…,” aliandika Masogange.


Post a Comment