MALAIKA MUSIC BAND IMEANZA VEMA SAFARI YAKE YA KUINGIA KWENYE ANGA ZA MUZIKI WA DANSI
MALAIKA Music Band imeanza vema safari yake ya kuingia kwenye anga za muziki wa dansi kwa kupata mahudhurio makubwa ambayo hayajawahi kuonekana hapo kabla katika ukumbi wa Mzalendo Pub. Ni funika bovu, show safi, waimbaji safi, wapiga vyombo safi.
Ukumbi umeshona ile mbaya kwa mara ya kwanza lile eneo la parking ya juu ya magari ilibidi lihamishwe na ukumbi uchukue nafasi hadi eneo hilo.
Christian Bella amethibitisha kuwa yeye ni mwimbaji bora, ni kama vile wanavyosema waswahili pembe la ngombe halijifichi – hakika uwezo wa Bella haujifichi.












Post a Comment