JESHI LA POLISI JIJINI MWANZA LAFANYA JARIBIO LA KUKABILIANA NA MAGAIDI
Wananchi
wakiwa eneo la Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza wakati wanausalama
wakifanya jaribio la uvamizi kuona uwezo na namna ya wananchi na jamii
kwa ujumla wanavyoweza kukabiliana na matukio ya aina hiyo.
Ikiwa ni mwezi mmoja na siku kadhaa zimepita tangu kutokea kwa tukio
la kigaidi la uvamizi wa maduka ya Westgate mjini Nairobi yaliyofanywa
na kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab, asubuhi ya leo Novemba 7 2013,
mamlaka za usalama mkoani Mwanza zimefanya uvamizi kwenye hoteli ya Gold
Crest ya jijini Mwanza.
Hali ilivyokuwa eneo hilo la uvamizi.
Uvamizi huo ambao kwa taarifa za awali kutoka katika vyanzo vyetu
lilikuwa ni jaribio kuona uwezo na namna ya wananchi na jamii kwa ujumla
wanavyoweza kukabiliana na matukio ya aina hiyo.Hata hivyo tukio hilo lililochukua muda wa saa nzima limeibua taharuki kwa wananchi waliokuwa ndani ya hoteli na nje ya hoteli hiyo jambo lililopelekea umati wa watu wengi kukusanyika kwa lengo la kujua nini kinachoendelea.
Hakika kwa utamaduni huu wa Watanzania kukimbilia kwenye eneo la tukio badala ya kukimbia sehemu salama kuna hatari ya watu wengi kupoteza maisha kama tukio kama hili likitokea katika mazingira ya uhalisia (tunaomba manani atuepushe na mabalaa ya namna hii).

Post a Comment