BREAKING NEWS: RAGE ASIMAMISHWA SIMBA
Alhaj Ismail Aden Rage
KIKAO
cha Kamati ya Utendaji ya Simba SC kilichokutana jana, kimefikia uamuzi
wa kumsimamisha Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage kwa
kukiuka taratibu na maadili ya uongozi.
Simba
SC imeitisha Mkutano na Waandishi wa Habari ambao utafanyika saa 5:30
makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam kuelezea kwa
undani suala hilo.
Wazi
hatua hii inazidi kuivuruga klabu, kwani tayari aliyekuwa Makamu
Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ naye amejiuzulu na nafasi yake
inashikiliwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Joseph Itang’are ‘Kinesi’.
Maana yake Simba SC inaendeshwa bila kiongozi Mkuu wa kuchaguliwa na hiyo inaweza kushinikiza uchaguzi haraka.
HABARI ZAIDI ZITAFUATIA BAADA YA MKUTANO WA KLABU NA WAANDISHI WA HABARI.

Post a Comment