REAL MADRID YAWAFUMUA AKINA DROGBA WIKI NZIMA NYUMBANI KWAO...BALE ANG'ARA, RONALDO ATISHA MBAYA
NYOTA
Gareth Bale ametokea benchi na kupikia mabao mawili Real Madrid
ikiitandika Galatasaray mjini Istanbul mabao 6-1 huku Cristiano Ronaldo
akipiga hat-trick yake ya 21 Bernabeu.
Bale aliwashuhudia Isco, Karim Benzema
na Ronaldo wakiiweka klabu yake mbele kwa mabao 3-0 kabla ya kuingia na
kutoa mchango wake kunenepesha ushindi.
Match ball's mine: Cristiano Ronaldo put the ball inside his shirt after netting a hat-trick in Istanbul
Kwanza, ilikuwa mpira wa adhabu wa winga huyo wa Wales uliomkuta Ronaldo, ambaye akaifungia bao la nne timu ya Carlo Ancelotti. Kisha akampa pasi Ronaldo, ambaye alimpasia pia Benzema kabla ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kufunga bao lake la pili katika mchezo huo.
Kwanza, ilikuwa mpira wa adhabu wa winga huyo wa Wales uliomkuta Ronaldo, ambaye akaifungia bao la nne timu ya Carlo Ancelotti. Kisha akampa pasi Ronaldo, ambaye alimpasia pia Benzema kabla ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kufunga bao lake la pili katika mchezo huo.
Isco alifunga dakika ya 33, Benzema 54 na 81 Ronaldo 63, 66 na 90, wakati bao la kufutia machozi la wenyeji lilifungwa na Bulut dakika ya 84. Didier Drogba alicheza kwa dakika 45 tu kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Amrabat.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas/Lopez dk14, Carvajal, Ramos, Pepe, Arbeloa, Modric/Illarramendi dk72, Khedira, Di Maria, Isco/Bale dk64, Ronaldo na Benzema Galatasaray: Muslera, Eboue, Chedjou, Nounkeu, Riera, Inan, Melo, Baytar/Bruma dk62, Yilmaz, Sneijder na Drogba/Amrabat dk46.
Katika
mechi nyingine, Man Utd imeshinda 4 -2 dhidi ya Bayer Leverkusen, Real
Sociedad imefungwa nyumbani 2-0 na Shakhtar Donetsk, FC Copenhagen
imetoa 1 - 1 na Juventus, Benfica imeifunga 2 - 0 Anderlecht,
Olympiacos imefungwa 4-1 nyumbani na PSG, Bayern Munich imeichapa 3 - 0 CSKA Moscow wakati Plzen imefungwa 3-0 nyumbani na Man City.

Post a Comment