KOMBE LA DUNIA 2014: IVORY COAST VS SENEGAL, MISRI VS GHANA, TUNISIA VS CAMEROON - NANI KWENDA BRAZIL?
MABINGWA wa soka wa
Afrika, Nigeria wamepangwa na timu isiyopewa nafasi sana, Ethiopia,
wakati Ghana imekabidhiwa shughuli pevu mbele ya Misri katika mechi za
mchujo za kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika
mwakani Brazil.
Droo ya mechi hizo imefanyika muda mfupi uliopita


Ivory
Coast vs Senegal,
Ethiopia vs Nigeria,
Tunisia vs Cameroon,
Ghana vs
Misri,
Burkina Faso vs Algeria.
Mechi za kwanza za mchujo huo
zinatarajia kufanyika kati ya Oktoba 11 na 15, wakati marudiano zitakuwa
kati ya Novemba 15 na 19 mwaka huu.
Post a Comment