KILICHOMUUA MSANII MALISA KINASIKITISHA SOMA HAPA.
TASNIA ya filamu Bongo imepata pigo lingine baada ya mwishoni mwa wiki
iliyopita kuondokewa na msanii aliyekuwa akichipukia kwa kasi
aliyefahamika kwa jina la Zuhura Maftah ‘Malisa’.
Malisa alifariki
dunia katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar baada ya kusumbuliwa
na uvimbe kichwani kwa takriban miezi mitatu.

Wakizungumza na gazeti
hili mara baada ya kifo hicho, baadhi ya wasanii wa filamu walielezea
masikitiko yao na kusema hakika wamemkosa msanii ambaye siku za baadaye
angekuwa moto wa kuotea mbali.
“Kifo chake kimetusikitisha sana,
Malisa alikuwa mmoja wa wasanii ambao walikuwa wakija kwa kasi,
amefariki dunia wakati ndiyo kwanza nyota yake ilikuwa imeanza kung’ara
lakini kazi ya Mungu siku zote haina makosa, akapumzike kwa amani,”
alisema mmoja wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Msanii
mwingine wa filamu ambaye huenda kifo hicho kimemgusa kuliko wengine ni
Yvonne Cheryl ‘Monalisa’ ambaye inadaiwa muda mfupi kabla ya Malisa
kufariki waliongea na kumwambia anaendelea vizuri.
Mmoja wa watu
waliokuwa wakimhudumia Malisa hospitalini hapo aliyefahamika kwa jina la
Vanitha alisema: “Siku ya kifo chake aliniambia nimpigie simu Mona
aongee naye kwani hajamuona siku hiyo, ilikuwa saa 12 jioni baada ya
kumaliza kumuogesha.
“Waliongea na kumwambia anaendelea vizuri.
Baada ya Malisa kumaliza kuongea na Mona niliondoka lakini nilipofika
Surender Bridge nikapata taarifa kuwa amefariki dunia,” alisema Vanitha.
Post a Comment