HIVI NDIVYO WAFUASI WA RAIS ASSAD WA SYRIA WANAVYOUAWA MBELE YA WANANCHI.
WATU wanaomuunga mkono Rais wa Syria, Bashir al-Assad, wamekuwa
wakikamatwa na kuuawa mbele ya wananchi. Mauaji yamekuwa yakifanywa kwa
njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukatwa shingo au viungo vya mwili
kwa kutumia majambia na silaha zingine.
Haya yote hufanyika mbele
ya watu wanaoshangilia na wengi wao wakiwa na silaha. Miongoi mwao ni
pamoja na watoto. Mauaji ya mwisho ambayo yalinaswa hivi karibuni ni
yale yaliyotokea katika mji wa Keferghan kaskazini mwa nchi hiyo.
Inasemekana mauaji hayo hufanywa na kundi la ISIS ambalo ni tawi la
Al-Qaeda linalompinga Assad na wanaofanyiwa mauaji hayo ni kundi
linalojulikana kama Shabiha (Mizimu) ambalo linamuunga mkono rais huyo.
Post a Comment