ALIYOSEMA MSANII DR CHENI BAADA YA KUTEULIWA KUWA BALOZI WA KAMPUNI MPYA YA SIMU.
Dr Cheni akiongea na millardayo.com amesema haya kuhusu ubalozi wake
na hiyo simu,”Simu inaitwa Pantech, ni simu mpya kabisa na ina operating
system ya Android version mpya. Ukizingatia sasa hivi internet ndiyo
kila kitu kwenye simu za mkononi, Pantech inatumia 4G na LTE kwenye
connection ya internet.
Kitu kingine kizuri ni kwamba simu hii inauwezo
wa kujichaji na nguvu za jua.
Sasa jua letu hatutalichukia tena na pia
ina camera nzuri ambayo inaitwa Spy camera yenye uwezo wa kupiga picha
mbali sana.”
Dr Cheni aliendelea kuongelea kuhusu mkataba wake na majukumu
yake,”Majukumu yangu hasa ni kuhakikisha simu hii watu wanatambua uwepo
wake. Matangazo na promotion zinapofanyika nitakuwa na shiriki
kikamilifu kabisa.
Wamenipa mkataba wa mwaka mmoja kwa sasa na swali
lako la thamani ya mkataba wangu naomba niweke kapuni kwasasa, ila
millardayo.com itakuwa ya kwanza kujua thamani yake muda wa kuweka wazi
ukifika.
Ninachoweza kukwambia hivi sasa ni bei tu ya simu hizi ambayo
ni Tsh 250,000 tu.”
Diamond,JB,AY,Mwana F.A,B12,Steve Nyerere ni Mzee Majuto baadhi ya
watu maarufu wa Tanzania ambao wanafanya kazi na kampuni tofauti kwa
ajili ya kutangaza bidhaa zao.

Post a Comment