MAN UNITED KUMPANDIA DAU BAINES BEKI WA EVERTON
KLABU ya Manchester United itampandia dau beki wa Everton, Leighton Baines hadi Pauni Milioni 15.
Baada ya kuipiga chini ofa yao ya awali
ya Man United ya Pauni Milioni 12, Everton imesema beki huyo wa kushoto
wa kimataifa wa England hauzwi.
Lakini United imepania kupanda dau hadi Pauni Milioni 20 katika kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28.
Atatua, Manchester? David Moyes anamtaka Baines awe chaguo lake la kwanza katika beki ya kushoto
Mrithi wa Moyes, Everton, Roberto
Martinez anataka kumbakzia beki huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 20
na klabu hiyo inataka kumpa Mkataba mpya ikimuongezea mshahara hadi
Pauni 70,000 wiki.
Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright
alielezea umuhimu wa Baines kwao, akisema: "Leighton ana Mkataba na
nimemuambia David usimfuate tena, ingawa hakuna cha kumzuia. Anajua
tunataka abaki,".
Mpango huu unamuweka shakani beki
Mfaransa, Patrice Evra juu ya mustakabali wake Old Trafford na wazi sasa
anaweza kuhamia Monaco au Paris Saint-Germain.
Nia: Mpango wa Moyes kutaka kumsajili beki wa Everton, Baines unaleta shaka juu ya mustakabali wa Patrice Evra

Post a Comment