MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho
ameuelezea msimu huu kwamba ni mbaya zaidi kwake katika maisha yake ya
soka baada ya kushuhudia kikosi chake kikitoka kapa kwa kukubali kipigo
cha mabao 2-1 kwenye muda wa nyongeza dhidi ya Atletico Madrid katika
mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme. Madrid
tayari walishalitema taji la La Liga kwa mahasimu wao Barcelona na
kuenguliwa na Borussia Dortmund katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya hivyo Kombe la Mfalme ndio ilikuwa karata ya mwisho kwa Mourinho
msimu huu kuondoka taji lakini nalo lilishindikana. Mourinho amesema kwa
makocha wengine nafasi ya pili aliyopo katika ligi, na kufika nusu
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na kucheza fainali ya Kombe la
Mfalme ni mafanikio lakini kwake umekuwa msimu mbaya zaidi. Kocha
huyo pia alikwepa swali kwamba msimu ujao ana mpango wa kutimkia klabu
ya Chelsea akidai kuwa kwasasa anachojua bado ana mkataba na Madrid, na
pia hajakaa chini na rais wa klabu hiyo kuzungumzia mstakabali wake wa
huko mbele.
Post a Comment