LULU AIBUA JIPYA HABARI YA MJINI.
NYOTA wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, ameibua
jipya ambapo kwa sasa habari ya mjini ni kwamba ana bwana mpya
aliyetajwa kwa jina moja la Junior, Amani limezinasa habari hizo.
Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, katika pozi na bwana wake mpya aliyetajwa kwa jina moja la Junior.
Ishu hiyo ambayo ndiyo gumzo midomoni mwa watoto wa mjini ilianza
kusambaa tangu Aprili 1, 2013 staa huyo alipoangusha pati ya
kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambayo ilichukua nafasi ndani ya
Ukumbi wa Hoteli ya Serena katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Maneno ya mjini yanasema kuwa staa huyo amekuwa akiweka picha yake akiwa
na Junior kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku wadau wakimpongeza
kwa kumtambulisha mpenzi wake huyo.
Mbali na picha ya Lulu akiwa na huyo Junior, ipo picha aliyopiga mama yake Lulu akiwa na kijana huyo katika pozi la kufanana na mwanaye.
Mbali na picha ya Lulu akiwa na huyo Junior, ipo picha aliyopiga mama yake Lulu akiwa na kijana huyo katika pozi la kufanana na mwanaye.
Chanzo chetu cha habari hii hakikuamini maneno
ya wadau wala ya mjini, juzi lilimsaka nyota huyo na kumuuliza kuhusu
madai hayo ya watu ambapo alikataa katakata kuwa na bwana mpya.
Msikie mwenyewe Lulu: “Junior si mpenzi wangu, ni rafiki tu na ana mchumba’ake, sema watu wamekuwa wakinihusisha naye ili niongee wakati mimi sitaki kabisa kuongelea kitu chochote hasa visivyo na maana kama hicho.”

Post a Comment