Chadema wamchangia mtoto upasuaji wa moyo.
Arusha.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Arusha,
kimetoa mchango wa zaidi ya Sh1.3 milioni kusaidia gharama za operesheni
ya moyo kuokoa maisha ya mtoto, Beatrice Shemtibuko (1.7), anayetakiwa
kupelekwa nchini India kwa matibabu.
Fedha hizo zilichangwa na
wafuasi wa chama hicho wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika
Viwanja
vya Shule ya Msingi Ngarenaro baada ya Mbunge wa Jimbo la Arusha,
Godbless Lema kumtambulisha jukwaani mama mzazi wa mtoto huyo, Selina
Peter aliyefika mkutanoni hapo kuomba msaada wa Dola 2,700 za Marekani
kwa wasamaria kufanikisha matibabu ya mwanaye.
Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Martin Sarungi alimkabidhi mama wa mtoto huyo hundi ya Sh 1.39 milioni alizosema ni mchango wa wananchi .
Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Martin Sarungi alimkabidhi mama wa mtoto huyo hundi ya Sh 1.39 milioni alizosema ni mchango wa wananchi .
Wenye nia ya
kuchangia matibabu ya mtoto huyo wanaweza kufanya hivyo kupitia mtandao
namba za simu 0757386623, 0655386623 akaunti namba 0142030004968 Benki
ya NBC Ltd.

Post a Comment