ad

ad

Zantel yapata Mkurugenzi mpya ni Pratap Ghose.

KAMPUNI ya simu za mikononi ya Zantel imemteua Pratap Ghose, kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni hiyo nchini.


Kabla ya uteuzi huo, Pratap ambaye ana miaka 18 ya uzoefu kwenye sekta mbalimbali ikiwemo mawasiliano alikuwa Makamu wa Rais wa Etisalat, uchumi na ukuzaji wa biashara kwa Kanda ya Afrika.

Pratap amewahi pia kushika nafasi mbalimbali ikiwemo Ofisa Fedha Mkuu wa kampuni dada ya Etisalat, India, pamoja na mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Atlantique Kanda ya Afrika Magharibi. Anachukua nafasi ya Ali Bin Jarsh ambaye ameiongoza kampuni ya Zantel kwa miaka miwili.

Mkurugenzi huyo mpya pia ana uzoefu mkubwa wa soko la Tanzania akiwa amefanya kazi kama mshauri wa Zantel na pia kwa kipindi cha miaka miwili amewahi kuwa Ofisa Fedha Mkuu wa Kampuni ya Tigo-Tanzania.

Akiwa Zantel, Pratap atakuwa na jukumu la kuongeza idadi ya wateja, pamoja na kusimamia ukuaji wa kampuni na vyanzo tofauti vya mapato.
Powered by Blogger.