BAO
la dakika za lala salama la Cesc Fabregas, jana limeipa Barcelona
ushindi wa 1-0 dhidi ya Levante siku ambayo Eric Abidal alicheza mechi
yake ya kwanza kwa dakika zote tisini tangu afanyiwe upasuaji wa ini. Huku
mfungaji tegemeo wa timu hiyo Lionel Messi akiwa nje kwa maumivu yake
ya nyama za paja la kulia ili awe fiti kabisa kabla ya kumenyana na
Bayern Munich katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa, safu ya
ushambuliaji ya Barcelona ilikosa makali yake mbele ya Levante hadi
Fabregas alipofunga dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho.Ushindi
huo unaisogeza Barcelona karibu kabisa na ubingwa wa La Liga, sasa
ikiwa inaongoza kwa pointi 13 zaidi zikiwa zimebaki raundi sita. Kwa
upande wa mahasimu wao Real Madrid nao walishinda mchezo wao kwa mabao
3-1 dhidi ya Real Betis na kukwea mpaka nafasi ya pili mwa msimamo wa La
Liga mabao ambayo yalifungwa na Karim Benzema ambaye alifunga mawili na
Metsu Ozil.
Post a Comment