Watu 50 wauawa katika milipuko kadhaa Iraq
Maafisa wa usalama na tiba wa Iraq wamesema kuwa, karibu watu 50
wameuawa na wengine 200 kujeruhiwa kufuatia milipuko kadhaa iliyotokea
leo kwenye maeneo tofauti ya nchi hiyo.
Katika mji mkuu Baghdad, milipuko 6 ya kutegwa kwenye magari
iliyolipuka katika vitongoji vitano vya mji huo imeua watu 8 na kujeruhi
wengine karibu 50.
Katika mji wa Tuz Khurmatu ulioko kilometa 175
kaskazini mwa Baghdad magari matatu yalilipuka na kuua watu 6 huku
wengine 60 wakijeruhiwa. Milipuko kama hiyo imetokea pia kwenye miji ya
Kirkuk, Hilla na Nasiriyah.
Milipuko hiyo imetokea nchini Iraq huku nchi hiyo ikijitayarisha nkwa
ajili ya uchaguzi wa Bunge unaotarahiwa kufanyika tarehe 20 Aprili
katika majimbo 12 kati ya 18 ya nchi hiyo.

Post a Comment