ad

ad

Rupia Banda akamatwa tena na kushtakiwa Zambia

Rais wa zamani wa Zambia, Rupia Banda amekamatwa tena mapema leo na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kuiba malori 9 ya serikali wakati alipokuwa ofisini.
Malori hayo yalitolewa kama msaada kwa serikali na shirika moja la ujenzi ambalo lilisaidia kujenga uwanja wa michezo wa Ndola.

Upande wa Mashtaka umesema kiongozi huyo wa zamani alikataa kukabidhi malori hayo kwa serikali na badala yake akayapeleka nyumbani kwake. Banda mwenye umri wa miaka 76 ameachiliwa kwa dhamana na mahakama imeamuru hati yake ya kusafiria itwaliwe.
Hii ni katika hali ambayo, kiongozi huyo bado anakabiliwa na mashtaka mengine ya utumiaji mbaya wa madaraka. Machi 25 rais huyo wa zamani wa Zambia alipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za ulaji rushwa ambapo korti iliahirisha kesi hiyo hadi baadaye mwezi ujao.
Powered by Blogger.