ad

ad

Wafanyabiashara Arusha wagoma kulipa kodi ya pango.


                            Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Afwilile Lamsy .
Wafanyabiashara zaidi ya 300 wa maduka yaliyopo katika stendi ndogo Jijini  Arusha wamegoma kulipa kodi mpya ya pango iliyotolewa na halamashauri ya Jiji hivi karibuni.
 

Wafanyabiashara hao wamedai kuwa  uongozi wa  Jiji  la Arusha umetoa  mkataba mpya na kiwango cha juu cha kodi ambayo sio halalali .
 

Kwa mujibu wa mkataba huo mpya wafanyabaishara hao wanatakiwa kulipa Sh.275,000 kwa mwezi badala ya Sh.60,000 wanazolipa siku zote.
 

Katibu wa wafanyabiashara hao Melance Kisoka alisema kuwa manispaa hiyo pia imefanya makosa ya kisheria kwa kutengeneza mkataba  mpya na kupandisha kodi  kwa kiwango cha juu ambacho hakiwezi kulipika.
 

“Hatufahamu ni wapi wametoa haya mahesabu kwamba tulipe kiasi hiki cha fedha na pia wameweka mkataba wa miezi minne  hatua ambayo ni kinyume na mazingira ya biashara na taasisi zinazotoa mikopo utawezaje kukopa pesa na kufanya biashara uweze kurejesha mkopo hakuna benki itakayoweza kukubali kitu kama hiki” alisema Kisoka
 

“Kwanza ieleweke wazi hatupingi kulipa kodi lakini kuna mambo ya msingi yanapaswa kuwekwa sawa ikiwemo kujua mmiliki halali  wa maduka kwa kuwa haya maduka tuliyajenga wenyewe ”alisema Kisoka.
 

Mfanyabiashara mwingine  Abraham  Chipaka  alisema kuwa hatua hiyo ni mbinu  chafu za manispaa ya jiji kutaka kuwapora maduka yao waliyojenga kwa nguvu zao.
 

Alipoulizwa kuhusu suala hilo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,  Afwilile Lamsy  alijibu kwa kifupi  kwamba anachojua walichukua hatua hiyo kwa kuzingat
Powered by Blogger.