SUAREZ AIOKOA LIVERPOOL KUZAMA KWA CHELSEA, AMNG'ATA IVANOVIC.
BADO kifogo tu kocha wa zamani wa
Liverpool, Rafael Benitez aibuke na ushindi katika mechi yake ya kwanza
dhidi ya timu yake hiyo ya zamani Uwanja wa Anfield, lakini mshambuliaji
wa Wekundu hao, Luis Suarez akazima ndoto hizo kwa kufunga bao la
kusawazisha dakika za lala salama.
Oscar alitangulia kuifungia Chelsea
dakika ya 26, lakini Strurridge akasawazisha dakika ya 52 kabla ya
Hazard kuifungia The Blues bao la pili kwa penalti dakika ya 57 na
Suarez akasawazisha dakika ya 90.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Reina,
Johnson, Carragher, Agger, Jose Enrique, Gerrard, Lucas, Downing/Shelvey
dk80, Henderson, Coutinho/Sturridge dk46 na Suarez.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Bertrand, Ramires, Mikel, Mata/Lampard dk90, Oscar/Moses dk83, Hazard/Benayoun dk78 na Torres.
Rufaa ya kifo: Luis Suarez akifunga kwa kichwa bao la kusawazisha kwa timu yake Liverpool dhidi ya Chelsea
Njaa? Suarez alimuuma Branislav Ivanovic kipindi cha pili.
Bao la kwanza: Oscar akiifungia Chelsea bao la kwanza kwa kichwa Uwanja wa Anfield

Post a Comment