
Mbunge Wa Arusha Mjini Godbless Lema Akiwatuliza Wanafunzi Wa Chuo Hicho
Vurugu kubwa zimeibuka chuo cha uhasibu cha Arusha baada ya mwanachuo kuchomwa kisu na mwanaakijiji na kufariki dunia....
Baada ya tukio hilo, wanafunzi walitoa taarifa kwa mkuu wa chuo lakini hakuwapa msaada wowote.
Walipokosa msaada,wanafunzi hao walianza kuandamana na taarifa zikafikishwa kwa mbunge Godbless lema ....
Mbunge
huyo bila hiyana akawasili na kufanikiwa kuwatuliza wanachuo hao
maana nyumbani kwa Godbless lema si mbali na chuo hicho ...

Baada
ya taarifa kumfikia Mkuu wa mkoa, ilimbidi aliwasili na kuanza
kuzungumza na wanachuo lakini baada ya kugundua uwepo wa Lema alianza
kuongea kwa lugha mbovu na ndipo wanachuo walipo kasirika na kuanza
kumpiga mawe.
Hali
ilipochafuka,FFU waliingia kazi ya kutuliza ghasia...Hali ni mbaya
sana lakini cha kushangaza askari mmoja aliwatonya wanachuo wamfiche
Lema
Godbless Lema anasakwa mpaka sasana hajulikani alipo baada ya wanachuo kumficha kusiko julikana. |
Post a Comment