Ukisoma hapa, utambaini mpenzi msaliti
Uaminifu ni mbolea katika mapenzi na usaliti ni sumu. Wengi wapo kwenye
uhusiano usiyo na afya kutokana na tamaa za pembeni. Kwamba mmoja
anashindwa kutosheka na aliyenaye, hivyo anakwenda kutafuta ‘urojo’ mtaa
wa pili.
Ipo tafsiri hii; Kumsaliti mwenzi wako maana yake umemdharau. Yaani umemuona ni mjinga wa mwisho kwenye mapenzi ndiyo maana ukaamua kuitoa sadaka heshima yake.
Jiulize; Yeye ndiye amezoea kukuona ukiwa katika hali zote, kesho unataka watu wengine wamtazame vipi ikiwa mwili wako umeutoa kwa mwingine? Inamaana hauna ‘uspesho’ tena kwake, anavyokujua na wengine ni hivyo hivyo.
Fumba macho utafakari; Anakujua ukiwa hauna nguo, lakini hicho si kitu ‘spesho’ tena, kwani mtaa wa tatu yupo mwingine anayekujua vilivyo unapokuwa umesaula. Heshima ya kweli ipo wapi?
Thamini utu wako; Anayetembea bila nguo siku zote anaitwa kichaa, wewe ambaye unakutana na huyu kesho yule uwekwe fungu gani? Muungwana hawezi kufurahia kitendo cha viungo vyake vya siri kuonwa hovyo!
Chukua ukweli huu; Ukiona mwenzi wako anateseka baada ya kujua umemsaliti, maana yake anaumizwa na kumbukumbu ya yale ambayo huwa mnayafanya faragha, halafu anafikiria hicho ndicho ulichokipeleka nje!
Kinachomtesa; Ule muonekano wako eneo la tukio, vitendo vyako kwake na ile ladha ambayo huwa anaipata kwako, halafu anajiona yeye si mali kitu tena kwa sababu vyote hivyo umempa mwingine. Heshima yake ipo wapi?
Tambua; Mapenzi ni kitu maalum, ya kwako na mwenzako yabaki kuwa yenu ndiyo maana mkaitwa wasiri. Wewe utakuwa na wasiri wangapi, ikiwa unashindwa kutulizana kwa mmoja? Unapata sifa gani ikiwa siri zako za chumbani wanazijua watu 20?
Uchunguzi unaonesha kuwa watu ambao waliwaamini mno wapenzi wao, ni hao hao waliofanya uamuzi mbaya baada ya kuwafumania au kubaini wanajihusisha kimapenzi nje ya uhusiano wao.
Kusaliti penzi ni kitu kibaya. Katika dunia ya sasa ambayo walimwengu wanapambana na maradhi,hupaswi kuwa na tamaa kwa kuhisi kuwa utapata vitamu pembeni.
Hata hivyo, muhimu ni kujua alama za mpenzi wako ili ukiona tofauti ujue kwamba huyo anakwenda tofauti. Ni dalili zipi ukiziona zinaweza kukupa mwanga wa kwamba mwenzako anakusaliti?
Mwanamke akiwa hivi ujue si mwema
Ghafla, anabadilika na kuchukua saa nne kujiandaa katika sehemu ya saa mbili. Hii ni njia ya kwanza, pia angalia mtindo wa nywele, ni za gharama na anaziweka maridadi! Anakwenda saluni mara kwa mara, anabadili manukato na mavazi!
Anatoka kwenda dukani mara moja lakini anavaa kama anakwenda ofisini au kwenye sherehe, huko anatumia saa mbili, akirudi anakupiga porojo kwamba alikutana na rafiki yake waliyepotezana miaka miwili iliyopita.
Simu yake ikiita ‘anapaniki’. Utamjua kwa jinsi atakavyokuwa anahangaika kupokea. Macho yake ni kipimo namba moja!
Hakubani, wala hajali unapomuaga kwamba unakwenda na rafiki zako mahali, pia ghafla atabadilika na kukuacha uwe huru nyumbani kufanya yale ambayo mwanzoni aligomba.
Hii haina maana ya asilimia 100 kwamba ukiona alama hizi ujue anakusaliti, bali zikupe kazi (assignment) ya kufanya kuchunguza nyendo zake, yaani uwe macho naye!
Mwanaume akiwa hivi ujue si mwema
Alikuwa anapenda kumzungumzia ‘mdada’ fulani wa kazini kwake lakini ghafla amekata, hamzungumzii tena.
Tabia yake imebadilika, anakwenda kazini mapema na achelewa kurudi. Hakuna maelezo ya kuongezeka kwa majukumu yake ya kazi wala nyongeza ya maslahi.
Anavaa vizuri akienda kazini kuliko anapokuwa na wewe, pia anakuwa makini kwa muonekano wake.
Anaanza kuahirisha mitoko yenu na kudai ana safari na wafanyakazi wenzake. Hakwambii wanakwenda wapi.
Elimu yake kuhusu wanawake inaongezeka, kuanzia wanavyovaa, mitindo yao ya nywele. Amewajuaje? Akili kichwani kwao!
Ananunua nguo zake peke yake na hakushirikishi.
Ukiona haya kwa mwenzako, ongeza umakini. Si kwamba ndiyo uthibitisho kuwa anakusaliti lakini zikupe mwanga na taa nyekundu ikuwake. Abiria chunga mzigo wako!

Post a Comment