ad

ad

KWANINI WAPENZI HUGOMBANA?

Kama mshauri wa masuala ya kisaikolojia nimekutana na wengi wanaolalamika wakisema “Tunapendana sana lakini tunaviugomvi vya mara kwa mara, Sijui ni kwanini hii hali, tunajaribu kuondokana nayo lakini tunashindwa”.

Katika makala hii ninajaribu kuonyesha baadhi ya sababu zinazofanya wapenzi au wanandoa wengi kugombana mara kwa mara ingawa viugomvi hivi havimaanishi kwamba hawapendani na sio kwamba kwa kugombana huku mara kwa mara wako tayari kuachana.

Sababu
Pale mpezi mmoja anaposhindwa kufanya yale yaliyotarajiwa na mwingine
Kila mmoja wetu ana picha akilini mwake inayomwonyesha ni jinsi gani mpenzi au mwenza bora anatakiwa awe, picha hii yamkini imechoreka akilini mwetu tangia utotoni. Bila kudhamiria maranyingi tunajikuta tunaanza kulinganisha kiletulichokuwa nacho akilini na kile kilicho dhahiri kinachotokea. Katika mapenzi kwa sasa. Maranyingi wakati tunapojikuta tunagombana ni kutokana na utofauti wa vile mpenzi wako anavyofanya na vile ulivyomtarajia akilini mwako awe.

Uhalisi unaotokea unapokuwa tofauti na tuliyotarajia, hisia zetu zina umizwa, chuki inaamka, maumivu yanaibuka na hivyo hasira na ugomvi huja.
Hasira hapa hutumika kama njia ya kumlazimisha mpenzi au mwenza wako kukaribia au kujaribu kuwa kama yule mpenzi bora uliyekuwa unamuwaza akilini mwako.
Ingawa maranyingine pamoja na hasira hizi yawezekana tusione hata chembe moja ya badiliko.

Wapenzi wengi huishi miaka mingi hususani kwenye ndoa nakuwa ndani ya chuki za aina hii na walioshindwa kukidhi haja za kila mmoja.
Pale unapokuwa na tofauti kali katika misimamo yenu
Misimamo hii ni zile Imani au vitu tunavyoviamini na vinavyotusaidia kuendesha maisha yetu ya kila siku.
Kila mmoja wetu anavimisimamo anavyovisimamia kila siku maishani, vitu ambavyo tunaviamini na tunavipa uzito watofauti vitu hivyo.

Mfano, Kama msimamo au Imani ya mmoja wenu ni kihifadhi fedha na mwingine ni kuzitumia lazima tofauti baina yenu itakuwa kubwa, kwasababu wakati mmoja anajitutumua kutafuta fedha na kuziweka kwa maendeleo mwingine anajitahidi kuzitumbua kwa matumizi yasiyo na msingi, hapa lazima moto uwake baina ya wawili hawa.
Kama mmoja anapenda kujinyenyekeza na anaamini kuwa mume au mpenzi wa kiume anatakiwa kunyenyekewa, na wakati mwingine anaamini katika usawa wa jinsia, lazima hapa ugomvi usiishe. Ugomvi unakuwa lazima katika wapenzi wa aina hii maana kila mmoja anaamini kitu ambacho ni cha tofauti kabisa na mwingine, na kila mmoja anajaribu kuhimiza kila anachoamini kifanyike.

Pale tunapotofautiana namna tunavyotafsiri mahitaji yetu ya kihisia
wengi wetu kama sio wote hupenda vitu vitatu toka kwa wengine, upendo, kutambuliwa na heshima. Ingawa tunajitahidi kutunza mahitaji yote matatu lakini moja lina yazidi mengine, hili ni hitaji la upendo au penzi toka kwa yule unayempeda. Tatizo linakuja kwamba penzi halishikiki kwahiyo ni ngumu kulipa picha fulani, ndiyo maana ninapomuuliza mwanaume yeyote, unajuaje kwamba mkeo anakupenda, swali hili linakuwa gumu sana kujibu.

Tofauti hutokea haswa pale tunapotofautiana kutafsiri jinsi ya kuelezea penzi. Wengine wanaka walione penzi kwa macho, waone wanavyopendwa, wengine wanataka wasikie jinsi wanavyopendwa na wengine wanataka wahisi vile unavyompenda, sasa kama wewe unaona kupenda kwa kweli lazima mtu aone penzi kwa macho, wakati yeye anaamni ni lazima asikie hilo penzi masikioni mwake basi mtatofautiana sana na hamtaisha kubishana.

Ndio maana wako wapenzi wanaoona wamependwa na kuthaminiwa pale tu wanapopewa vitu vya thamani au kufanyiwa suprize, wakati wengine hutaka wasikie maneno kama “nakupenda” “I love u” “Umependeza” ndio wajue wanapendwa, hata kama hajapewa kitu chochote. Wapo ambao wanataka kuguswa, kukumbatiwa na wapenzi wao na katika hali hii watahakikisha kuwa wanapendwa. Jiulize sasa, wewe penzi unalitazamaje? Nini kifanyike ili uone kama unapendwa.

Pale ambapo ujumbe uliokusudiwa kutumwa sivyo anavyopokelewa
Magomvi mengi tena makali hutokea baina ya wapenzi wengi pale ambapo mmoja anatuma ujumbe fulani au kusema kitu fulani na yule anayepokea msikilizaji anahisi kama ameelewa na kuanza kutenda kumbe anatenda tofauti. Pasipo kuuliza aeleweshwe anafanya kile alicho au anachokiwaza akilini mwake kuwa ndicho sahihi kwa jinsi alivyokitafsiri.

Mfano, mpenzi wa kiume anesema “njoohapa” Mpenzi wakike mara anajibu “kwani nimefanyanini?” Anajibu hivi kutokana na kuhisi kuwa sauti hii iliyomwita ni yashari, kumbe sivyo awazavyo mpenzi wa kiume. Najua jinsi alivyoita yaweza maanisha anahasira na wewe, lakini pia yaweza maanisha amekasirishwa na kitu au vitu vingine. Chakufanya hapa, jifunze kuhakikisha kile ulichosikia au unachohisi umekielewa kabla hujarukia katika kutafsiri isiyvo sahihi.
Powered by Blogger.