RAYUU: SIMU IMEVUJISHA PICHA ZANGU CHAFU.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Alice Bugenzi ‘Rayuu’ amejutia
kitendo chake cha kupiga picha za utupu kwenye simu yake ya mkononi na
kueleza kuwa, kuibiwa kwa simu hiyo ndiko kulikosababisha matatizo kwake
na kwa familia yake.
Akifungukia
suala hilo juzikati kupitia mtandao wa Facebook kwa lengo la kuomba
msamaha kwa mashabiki, Rayuu alisema hakuwa na nia ya kujipiga picha
hizo na kuzisambaza kwa lengo la kutafuta umaarufu ila ilitokea hivyo
baada ya kupoteza simu yake ya mkononi.
“Mashabiki wangu naombeni
msamaha kutokana na kusambaa kwa picha zangu chafu, tambueni kuwa
haikuwa dhamira yangu bali ilitokea baada ya simu yangu ya mkononi
kupotea,” alisema Rayuu.

Post a Comment