Ivory Coast yaiomba UN iipatie ndege zisizo na rubani
Ivory Coast imeuomba Umoja wa Mataifa
utumie ndege zisizo na rubani katika mpaka wa nchi hiyo na Liberia.
Youssoufou Bamba, Balozi wa Ivory Coast katika Umoja wa Mataifa amesema
kuwa serikali ya nchi hiyo inauomba Umoja wa Mataifa utumie ndege zisizo
na rubani ili kufuatilia harakati za makundi yenye silaha kwenye mpaka
wa nchi hiyo na Liberia.
Bamba amesema utumiaji wa ndege zisizo na
rubani katika maeneo ya mpaka wa Ivory Coast na Liberia utawazidishia
uwezo askari jeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana
na harakati za makundi yenye silaha katika maeneo hayo. Hivi karibuni
Ivory Coast iliongeza idadi ya wanajeshi wake katika mpaka wa nchi hiyo
na Liberia kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi ya makundi yenye
silaha yanayoendesha hujuma katika maeneo ya mpaka wa nchi mbili hizo.

Post a Comment