Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba
"Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama
yetu mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma
haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu.
Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi. Nisingependa
kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni mama
wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule. Matukio ya
namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake litashughulikiwa kama
yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya Watanzania. Polisi
wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka zitachukuliwa.
Ushauri- tuwe makini na "Agente provocatuers" au in English "provocation
agents" nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against
provocations. Nadhani mmenipata"
Nawatakia Kila la kheri katika
kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa
Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Post a Comment