WOLPER, HARTMANN WAPATA AJALI
Issa Mnally na Richard Bukos
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amenusurika kufa ajalini baada ya gari lake kugongana na gari lingine.
Tukio
hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar, jirani
na nyumba ya staa mwenzake, Wema Sepetu ambapo Wolper aliyekuwa
akiendesha gari lake aina ya Toyota-Brevis Saloon alivaana uso kwa uso
na gari lingine aina ya Toyota-Nadia.
Kwenye ajali hiyo, gari la Wolper lilibondeka mbele na kuvunjika kioo cha pembeni (side mirror).
“Nilikuwa na mdogo wangu tunaelekea gereji kufuata gari langu, hili nililopata nalo ajali, siyo la kwangu hata sijui itakuwaje!” alisema Wolper.
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amenusurika kufa ajalini baada ya gari lake kugongana na gari lingine.
Kwenye ajali hiyo, gari la Wolper lilibondeka mbele na kuvunjika kioo cha pembeni (side mirror).
Wolper.
Akizungumza na mwandishi wetu, Wolper alithibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kumshukuru Mungu kwa kumnusuru kwani hakuumia popote.“Nilikuwa na mdogo wangu tunaelekea gereji kufuata gari langu, hili nililopata nalo ajali, siyo la kwangu hata sijui itakuwaje!” alisema Wolper.
Hartman Mbilinyi.
Wakati huohuo, Hartman Mbilinyi ambaye ni prodyuza wa filamu,
Jumatatu usiku alipata ajali baada ya gari lake kugongana na pikipiki
wakati akirudi nyumbani kwake, Tegeta.
Post a Comment