Vijana watakiwa kutumia Teknohama kujiajiri
MAKAMU wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, amewataka vijana hapa nchini
kutumia taaluma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA)
kujiajiri. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, alipofanya ziara
katika Taasisi ya Atamizi ya Biashara (DTBI) kwa ajili ya kupata taarifa
mbalimbali.
Alisema teknolojia iliyopo katika dunia ya sasa ndio mkombazi wa vijana wengi wanaojituma katika masomo ya sayansi na kupambanua mambo kwa vitendo.
“Unaweza kutumia teknohama katika nyanja nyingi kama vile kuzalisha mazao na kuwasiliana na mteja moja kwa moja na ukauza hata nje ya nchi na kupata faida kubwa,
“Vile vile itaongeza ufanisi na mzalishaji atapata tija zaidi na kujikuta uchumi wa mtu mmoja mmoja unakua, hatimaye Taifa zima kwa ujumla,” alisema Dk. Bilal.
Aliwataka wanafunzi waliopo shuleni kujikita zaidi katika masomo ya sayansi na kufanya utafiti kwa ajili ya kuwafikisha katika soko zuri la ajira.
“Katika hatua hii, tumeona ni jinsi gani utaalamu wa masomo ya sayansi yanavyopanuka, hivyo kufanya masomo ya sayansi yakue na kuhamia katika damu ya Watanzania,” alisema Dk. Bilal.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DTBI, Aape Pohjavirta, alisema zipo changamoto nyingi zinazoikabili taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na fikra nyingi za vijana kutaka kuajiriwa badala ya kujiajiri wenyewe kutokana na elimu au mafunzo waliyonayo.
Alisema nyingine ni sheria ya ununuzi kutotoa nafasi kwa wabunifu na wagunduzi katika Tehama, isiyosaidia wajasiriamali wa kizalendo na Watanzania kupata kazi.

Post a Comment