ROBIN VAN PERSIE KUZEEKEA MANCHESTER UNITED
ROBIN VAN PERSIE anataka kuichezea Manchester United kwa maisha yake yote yaliyobaki katika soka.
Mholanzi
huyo alihamia Old Trafford kutoka Arsenal kiangazi kilichopita baada ya
miaka nane akiwa na timu hiyo ya London Kaskazini.
Van
Persie amekuwa na mwanzo wa kishindo United, akifunga mabao 23 katika
mechi 31 za kwanza kukisaidia kikosi chake kuongoza Premier League.
Shabaha
ya nyota huyo wa miaka 29 ilipotea katika mechi saba za mwisho akiwa na
United, lakini ‘alifufuka’ na kuipigia mabao matatu Uholanzi katika
mechi mbili za hivi karibuni na kumpita gwiji Johan Cruyff katika chati
ya vinara wa kucheka na nyavu wa muda wote kwa timu hiyo ya taifa.
Van
Persie aliliambia gazeti la Voetbal: “Miaka ijayo ni Manchester United.
Na labda muda mrefu. United itakuwa klabu yangu ya mwisho.”
Amesema kila siku anakutana na changamoto mpya United, huku maendeleo yake yakizidi kusonga.
Mkataba
wa sasa wa Van Persie utafika mwisho akifikisha umri wa miaka 33,
lakini akiwatumia Giggs mwenye miaka 39 na Scholes, 38 kama kigezo,
mshambuliaji huyo nae anaweza kuongeza maisha yake Old Trafford.
CHANZO CHA HABARI NI SALUTI 5

Post a Comment