RAIS KIKWETE AWAONGOZA VIONGOZI KUMUAGA ALIYEKUWA MBUNGE WA CHAMBANI, SALIM HEMED KHAMIS
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mstaafu,
Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli ya kuaga mwili
wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani
Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye
Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka
kwenye ukumbi wa Karimjee baada ya kushiriki katika shughuli za kuaga
mwili wa marehemu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba,
Salim Hemed Khamis (CUF), aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili
Waombolezaji
wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF,
aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye
gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea Pemba kwa
maziko, yatakayofanyika leo.



Post a Comment