Pope kutawazwa rasmi Jumanne
Kanisa Katoliki linatarajiwa kuwakaribisha viongozi mbalimbali
duniani watakaohudhuria misa ya kutawazwa kwa Papa Francis,
wakati akianza wadhifa wake rasmi hapo kesho, Jumanne.
Hafla hiyo
inatarajiwa kuwa kinyume na hali ambayo kwa kawaida inahusiana
na matukio makubwa katika Kanisa hilo, kutokana na kiongozi huyo
wa Kanisa Katoliki alivyojionyesha katika siku chache za kwanza
kuwa mtu wa kawaida, akiwa papa wa kwanza kutoka eneo la
Amerika ya Kusini.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Waziri Mkuu Mariano Rajoy
wa Uhispania na mwenzake kutoka Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, ni
miongoni mwa viongozi wa juu wa Ulaya wanaotarajiwa kuhudhuria,
pamoja na Rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy na Rais
wa Halmashauri ya Umoja huo, Jose Manuel Barosso. Makamu wa
Rais wa Marekani, Joe Biden, ambaye ni Mkatoliki, amewasili jana
kuiwakilisha nchi yake katika sherehe hizo. Jana mchana, Papa
Francis aliwahutubia watu 150,000 waliokusanyika katika uwanja
wa Mtakatifu Petro.

Post a Comment