Mawakili wa Kenyatta wataka kesi ifutwe
Mawakili wanaomuwakilisha rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta,
kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, leo hii
watawakilisha ombi la kuitaka Mahakama hiyo kufuta mashitaka dhidi
ya kiongozi huyo.
Kesi dhidi ya Kenyatta, kwa madai ya uhalifu dhidi
ya ubinadamu kuhusiana na mauaji baada ya uchaguzi nchini Kenya
mwaka 2007, imeingia katika utata zaidi kutokana na ushindi wake
katika uchaguzi uliofanyika kwa amani mapema mwezi huu.
Kesi hiyo
pia ni mtihani mkubwa kwa Mahakama hiyo, ambayo iliundwa karibu
muongo mmoja uliopita kama mahakamaya kwanza ya kudumu
duniani inayowahukumu wahalifu wa kivita, lakini hadi sasa ikiwa
imeweza kutoa hukumu moja tu.
Kenyatta pamoja na mkuu wa
zamani wa utumishi wa umma, Francis Muthaura, walikuwa miongoni
mwa watuhumiwa sita ambao awali walifunguliwa mashtaka na
mwendesha mashtaka mkuu wa ICC kwa uchochezi katika ghasia
baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, ambapo karibu watu 1,200
wameuwawa. Jumatatu iliyopita, mwendesha mashitaka mkuu Fatou
Bensouda, aliondoa mashitaka dhidi ya Muthaura, ingawa alisema
kuwa uamuzi huo usingelikuwa na athari kwa kesi ya Kenyatta.

Post a Comment