Polisi Mkoa wa Manyara inamsaka Mbunge wa Viti wa Mkoa wa Manyara(Chadema ),Rose Kamili
Polisi Mkoa wa Manyara inamsaka Mbunge
wa Viti wa Mkoa wa Manyara(Chadema ),Rose Kamili pamoja na watu wengine
wanne kwa tuhuma za kufunga ofisi ya kijiji cha Basotu kwa zaidi ya wiki
moja sasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alisema jana kuwa wanamsaka mbunge huyo,pamoja na wenzake ili watowe maelezo kuhusiana na tukio hilo kabla ya kufikishwa mahakamana.
Mbunge Kamili alipoulizwa jana kuhusiana na kusakwa huko, alikiri kupata taarifa lakini akasema,kama polisi wanamuhitaji wamfuate nyumbani kwani wanapajua.
Hata hivyo, alisema uamuzi wa kufungwa ofisi hiyo, yalitolewa kwenye mkutano wa mkuu wa kijiji,kutokana na kupinga unyanyasaji wa viongozi wa kijiji, kutosoma mapato na matumizi tangu mwaka 2007 na pia kuwataka wafike Basotu viongozi wa wilaya.
Wananchi 365 walioshiriki mkutano mkuu huo wa
kijiji, licha ya kufunga ofisi hiyo pia walichagua vijana waliopitia
mafunzo ya mgambo kulinda ofisi hizo hadi muafaka utakapopatikana.

Post a Comment