MANCHESTER UNITED YATANGULIA NA BAISKELI YA MBAO.
WAKICHEZA
soka bovu, Manchester United wameshindwa kulinda magoli yao mawili ya
kipindi cha kwanza na kuruhusu Chelsea kuyakomboa kipindi cha pili
katika mechi ya robo fainali ya kombe la FA.
Dakika ya 5 ya mchezo Javier Hernandez
anakimbilia pasi ndefu ya Michael Carrick na kuupiga kichwa, mpira
unakwenda moja moja wavuni na kuandika bao la kwanza.
Wayne
Rooney akatupia bao la pili dakika ya 11 baada ya kupiga mpira wa
adhabu ulioambaa ambaa juu ya vichwa vya mabeki wa Chelsea na kumfanya
kipa Cech achelewe kuchukua hatua na kuacha mpira ukitinga wavuni.
Hernandez akishangilia goli la kwanza la United
Wayne Rooney anapiga la pili
Adhabu hiyo ilitokea baada ya mshambuliaji Victor Moses kumpiga kibega Luis Nani.
Baada
ya hapo Manchester ilipata nafasi chache za kufunga lakini umakini
mbovu wa washambuliaji wake ukafanya matokeo yabakie 2-0 hadi mpumziko.
Rooney akisherehekea goli lake
Kipindi cha pili Chelsea waliendelea kuwabana United na kuwalazimisha warudi nyuma kuhami lango lao.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Rafa Benitez katika dakika ya 52 yaliinufaisha Chelesea.
Benitez aliwatoa Frank Lampard na Victor Moses nafasi zao zikichukuliwa na Eden Hazard na John Obi Mikel.
Hazard
akiwa upande wa kushoto akapokea pasi ya Juan Mata, akauchonga mpira
uliokwenda kwenye nyuzi 90 upande wa kulia na kuandika bao la kwanza.
Mabadiliko ya Manchester kumtoa Hernandez na kumwingiza Van Persie dakika ya 62 hayakuizuia Chelea kuandika bao la kusawazisha.
David
Luiz alichukua mpira na katikati ya uwanja na haraka haraka akampa pasi
Demba Ba aliyempatia mpita Hazard aliyezunguka na kumpelekea mpira
Ramires aliyekuwa kando ya beki John Evans.
Hazard akipewa tano na wachezaji wenzanke ngoma 2-1 hiyo
Ramires akageuka na kuachia mkwaju wa chini chini wa yadi 16 uliompita kipa De Gea na kufanya matokeo yawe 2-2.
Ramiressssssss 2-2
Dakika za lala salama United walinusurika mara mbili baada ya De Gea kupangua mashuti ya Mata na Ashley Cole.
Mshindi wa mechi yao ya marudiano atakutana na Manchester City katika hatua ya nusu fainali.
Man Utd:
De Gea, Da Silva, Evans, Ferdinand, Evra, Carrick, Cleverley, Nani
(Valencia 45), Kagawa (Welbeck 76), Rooney, Hernandez (van Persie 62).
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Cole, Ramires, Lampard (Mikel 52), Moses (Hazard 52), Mata, Oscar, Ba (Torres 77).

Post a Comment