ad

ad

MANCHESTER UNITED YAANGUSHA KARAMU NZITO, CHELSEA YACHARUKA

MANCHESTER UNITED ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani, imeipa kipigo kizito Norwich City na kuzidi kujiimarisha kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza.
 United imevuna ushindi wa mabao 4-0 matatu kati yake yakiwa yamefungwa na kiungo Shinji Kagawa huku bao la nne likiwekwa kimiani na Wayne Rooney.

Iliwachukua United hadi dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza kupata goli la kwanza lililoanzia kwa Robin Van Persie kabla ya kumfikia mfungaji.
Kagawa akafunga tena katika dakika za 76, 82 na 87 kabla ya Rooney kuhitimisha karamu hiyo katika dakika ya 90.

Naye mshambuliaji Demba Ba aliipatia Chelsea goli pekee katika dakika ya 28 na kuipa timu yake pointi tatu muhimu dhidi ya West Bromwich.
Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa leo ni kama ifuatavyo:
Chelsea 1 - 0 West Bromwich A.
Everton 3 - 1 Reading
Manchester U. 4 - 0 Norwich C.
Southampton 1 - 2 Queens Park R.
Stoke C. 0 - 1 West Ham U.
Sunderland 2 - 2 Fulham
Swansea C. 1 - 0 Newcastle U.
Marouane Fellaini celebrates
Fellaini akishangilia moja ya mabao ya Everton dhidi ya Reading
Powered by Blogger.