BARCELONA SI LOLOTE KWA REAL MADRID
Sergio
Ramos amefunga la dakika ya 82 kufuatia kona ya Luka Modric na kuipa
Real Madrid ushindi wa 2-1 dhidi ya Barcelona katika mechi kali ya ligi
kuu ya Hispania.
Huo unakuwa ni ushindi wa pili wa Real Madrid dhidi ya Barcelona ndani ya siku tano.
Karim
Benzima alikuwa wa kwanza kuitanguliza mbele Real Madrid kwa bao lake
la dakika ya 6 kabla ya Lionel Messi hajasawazisha dakika ya 18 likiwa
ni goli lake la 18 katika mechi dhidi ya Real Madrid.
Kwa
bao hilo Messi sasa amefikia rekodi ya mkongwe wa Real Madrid Alfredo
Di Stefano ambaye nae alitupia magoli 18 katika mechi zilizozikutanisha
timu hizo.
Wakiwa
wanajiandaa na mechi ya ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester United
Jumanne ijayo, Real Madrid ilimpuzisha nyota wake Cristiano Ronaldo hadi
dakika ya 58 alipoingizwa ili kuongeza nguvu.
Baada ya mchezo kipa Victor Valdes alilimwa kadi nyekundu baada ya kutoa lugha chafu kwa mwamuzi.


Post a Comment