ad

ad

MANCHESTER CITY YAFA KIFO CHA MENDE YAPIGWA 2-0 NA EVERTON


VERY GOODISON ... Leon Osman celebrates his stunner
LONDON, ENGLAND
EVERTON imeifanyia kitu mbaya Manchester City katika harakati zao za kutetea ubingwa wa Premier League baada ya kuichabanga mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Goodison Park.
WHAT A STRIKE ... Leon Osman unleashes a thunderbolt
Osman akiandika bao la kwanza
Everton waliodhibiti eneo la kiungo walipata goli la kwanza kupitia mkwaju wa mbali wa Leon Othman katika dakika ya 32.
Dakika ya 62 Everton wakapata pigo baada ya kiungo wake Steven Pienaar kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano.
YOU'RE OFF ... Referee Lee Probert gives Steven Pienaar his marching orders
Steven Pienaar akilambishwa kadi nyekundu
City walitafuta goli la kusawazisha kwa udi na uvumba huku wachezaji wake Carlos Teves, Dzeko, Silva na baadae Nasir wakihaha huku na kule.
Lakini wenyeji hao waliopata mzuka wa kumaliza kwenye timu nne za juu baada ya kupata pointi tatu, walicheza ‘jihadi’ huku kipa wa akiba, Jan Mucha akiokoa mabao ya wazi kabla shuti la mwisho kutoka kwa Jelavic kuwahakikishia ushindi.
City walinyimwa penalti dakika za mwisho baada ya refa Lee Probert kutoa nje ya eneo la hatari mpira na kuamuru adhabu ya ‘frikiki’ baada ya Marouane Fellaini kuushika, ingawa tukio hilo lilitokea ndani ya boksi.
Dakika 90 za kawaida zikamalizika na kuingia dakika 3 za nyongeza.
Katika dakika ya mwisho kabisa ya muda huo wa nyongeza, Marouane Fellaini akachukua mpira kwenye eneo la goli lake akikiambia nao hadi jirani na 18 ya City, akammegea pasi Nikica Jelavic.
NIKKED IT ... Jelavic scores in injury time
Jelavic akijikunjua na kufunga bao la pili
Jelavic aliyeingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya Anichebe, hakufanya ajizi akaiahadaa beki ya City na kuachia mkwaju wa juu uliokwenda moja kwa moja wavuni.
Powered by Blogger.