ESTELINA Sanga ‘Linah’ na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Amini Mwinyimkuu wamenaswa katika pozi jipya la kimahaba zaidi.
Picha hiyo inayowaonesha wawili hao wakiwa ndani ya gari huku
mwanadafada akimbusu Amini, imedakwa juzikati katika mtandao wa BBM,
ambapo wadau wanaotumia mtandao huo aliwapongeza kwa kurudiana.
Amani lilimtafuta Linah, alipopatikana alijibu kwa kifupi kwamba hana
tatizo na Amini hivyo yupo huru kwa lolote mbele yake na wanafanya naye
kazi kwa karibu. Kwa upande wake Amini, alipoulizwa juu ya ishu
hiyo alitiririka: “Linah ni mtu wangu hivyo sina ubaya naye kwa kila
kitu atujawahi kugombana wala kusutana picha zisiwashtue watu,” alisema
Amini.
Post a Comment